![]() |
| Tundu Lissu |
Pia Mahakama imeamuru itolewe hati ya kuwaita wadhamini
wa Lissu, ambao ni Robert Katula na Ibrahim Ahmed wakajieleze kwa nini wasilipe
fungu la dhamana kutokana na kwamba Mbunge huyo amekuwa akikiuka masharti ya
dhamana.
Wakati hayo yakiendelea Dar es Salaam, Mbunge wa Arusha
Mjini, Godbless Lema naye amekamatwa na polisi waliomsafirisha kutoka Dodoma hadi
Arusha ambako anashikiliwa kwa mahojiano kwa tuhuma za uchochezi, akitarajiwa
kufikishwa mahakamani.
Hati ya kukamatwa kwa Lissu ilitolewa jana na Hakimu Mkazi
Mkuu, Thomas Simba, baada ya kubaini kuwa Mbunge huyo hayuko kizimbani, ndipo
alipotaka kujua kwa nini hayupo, kwa sababu hakuna ruhusa yoyote aliyopokea.
Mdhamini wa Lissu, Katula alimweleza Hakimu kuwa Mbunge
huyo amekwenda kwenye kesi ya uchaguzi, Mahakama Kuu ya Mwanza.
Kauli hiyo ilimkasirisha Hakimu Simba akasema: "Kama
tusingempa dhamana angekwenda kusikiliza kesi hiyo saa ngapi? Kwa sababu
Mahakama Kuu ya Mwanza amesimama kama wakili na huku ni mshitakiwa na anajua
kabisa dhamana inatolewa kwa masharti.
"Kwa nini anafanya hivi, kwa sababu mahudhurio yake
yamekuwa mabovu ni dharau au nini? Alitakiwa kutumia busara kuomba ruhusa na si
kuondoka bila taarifa," alisema Simba.
Katula alidai kuwa Lissu alimwambia aliandika barua ya
ruhusa ya moja kwa moja, hali iliyomfanya Hakimu huyo kushangaa na kumweleza
mdhamini huyo kuwa hakuna ruhusa ya jumla.
Hakimu Simba alimgeukia Wakili wa Serikali, Patrick Mwita
na kumwuliza anasemaje kuhusu Lissu kukiuka masharti ya dhamana ndipo alipoomba
hati ya kukamatwa kwa mshitakiwa itolewe.
"Hati ya kukamatwa kwa Lissu itolewe bila sababu
yoyote wala kujitetea na samansi za wadhamini Katula na Ahmed wajieleze kwa
nini wasilipe fungu la dhamana, kutokana na kwamba waliyemdhamini amekuwa
akikiuka masharti," alisema Simba.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi Novemba 21 itakapotajwa. Si
mara kwanza Lissu kukosekana mahakamani bila taarifa, alishawahi kwenda
Ujerumani kwa matibabu bila kutoa taarifa, ambapo wakati yote hayo yanaendelea,
mawakili wake hawakuwapo.
Washitakiwa wengine kwenye kesi hiyo ni Mhariri Mkuu wa Gazeti
la Mawio, Simon Mkina, Mhariri Jabir Idrisa na
Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob.
Ilidaiwa kuwa Januari 12 hadi 14, Dar es Salaam, washitakiwa
Jabir, Mkina na Lissu, waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye
kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar’.
Katika
hatua nyingine, Mbunge Lema, anashikiliwa katika mahabusu ya Polisi ya Kituo
Kikuu cha Polisi Arusha kwa mahojiano akidaiwa kutoa lugha za uchochezi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, Lema anashikiliwa hadi Jeshi hilo litakapomaliza mahojiano naye kuhusu tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi na baada ya kumalizika kwa mahojiano hayo atafikishwa mahakamani.
Kamanda Mkumbo alisema Lema amekuwa akitoa lugha za uchochezi na kuzirudia kila mara, hivyo wameona vema wamkamate wamhoji ili aweze kufafanua.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, Lema anashikiliwa hadi Jeshi hilo litakapomaliza mahojiano naye kuhusu tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi na baada ya kumalizika kwa mahojiano hayo atafikishwa mahakamani.
Kamanda Mkumbo alisema Lema amekuwa akitoa lugha za uchochezi na kuzirudia kila mara, hivyo wameona vema wamkamate wamhoji ili aweze kufafanua.
“Juzi tulimkamata akitoka Dodoma na tulifanya naye mahojiano na kumwachia kwa dhamana, lakini kuna baadhi ya makosa hatukuwahi kumhoji, sasa tumeamua kumhoji kwa mara nyingine,” alisema.
Hata hivyo, alipotakiwa kutaja maneno ya uchochezi aliyotamka Lema, Kamanda Mkumbo hakuwa tayari kuyaweka hadharani akisema kufanya hivyo ni kuharibu ushahidi na pia si sheria kwa suala ambalo bado liko kwenye uchunguzi.
Hata hivyo, Novemba mosi Kamanda Mkumbo akiwa anazungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, alitaja maneno ya uchochezi anayodaiwa Lema kuyataja kuwa ni:
“Mheshimiwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiendelea kukandamiza demokrasia,
siasa za ukandamizaji Taifa litaingia katika umwagaji wa damu, nchi hii
inaandaliwa kwenda katika utawala wa kidikteta,”.
Facebook Blogger Plugin by Tanzaniastar







Kweli siasa ni mchezo mchafu
ReplyDelete